VICTOR WANYAMA AKARIBIA KUTUA TOTTENHAM HOTSPURS

Kiungo mkabaji Wa kimataifa wa Kenya anayeichezea Southampton ya England Victor Wanyama anatarajia kutangazwa kuwa mchezaji mpya wa Tottenham Hottspurs pindi tu atakapokamilisha dili lake la kujiunga na Spurs.




Wanyama mwenye miaka 24 amebakiza mwaka mmoja wa kuichezea Southampton na tayari amekataa ofa ya mabingwa wa ligi kuu Leicester City ambayo imekua ikimwania na anataka kuungana tena na kocha wake Mauricio Pochettino ambaye anaifundisha Tottenham hivi sasa.

Kiasi cha paundi milioni 11 kimetajwa kama ada ya uhamisho wa nyota huyo akitarajiwa kusaini mkataba wa miaka minne.

No comments

Powered by Blogger.