UCHAGUZI MDOGO WA WAJUMBE WA BODI YA STAND UNITED KUFANYIKA JUNI 24.

Klabu ya Stand United ya Mjini Shinyanga inayodhaminiwa na kampuni ya uchimbaji madini ya ACACIA Imetangaza tarehe 24 Juni 2016 (Ijumaa wiki hii) kuwa siku ya kufanyika uchaguzi mdogo wa wajumbe wawili wa bodi ya Wakurugenzi wa klabu.




Muundo wa klabu hivi sasa unaeleza kwamba kutakua na bodi ya Wakurugenzi itakayokuwa na wajumbe 10 na mpaka sasa bodi hiyo ina tayari wajumbe 8 hivyo uchaguzi utakaofanyika utakua ni wa kujaza nafasi mbili zilizokua wazi.

Jumla ya wanachama 11 wamejitokeza kuchukua na kurudisha fomu tayari kwaajili ya uchaguzi huo

Wanachama Waliochukua na kurudisha fomu ni

1. MAKA MAULIDI MATETE
2. JOHN MAKOE SOSPETER
3. HAMIS HASSAN SHABAN
4. HAMAD MUSSA
5. PETER KABANZA
6. ISIKE ATHUMAN
7 KIBAGO MSOMI BWANA
8 SELEMAN EDSON
9. PELO SADALA
10. MANENO YAHYA
11. ABOUBAKAR NASSOR ABDALLAH


Imetolewa na 
ALEXANDER SANGA 
MKURUGENZI WA HABARI NA MAWASILIANO 
STAND UNITED COMPANY LIMITED 
0715052491

No comments

Powered by Blogger.