TUWASAIDIE SERENGETI BOYS HAKIKA TATIZO LAO NI TATIZO LA TAIFA ZIMA.
Na: Ayoub Hinjo
Hongera kwa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 "Serengeti Boys" kwa ushindi dhidi ya Shelisheli. Ushindi wa magoli 3 haukuwa wa haki kwa timu hiyo ambayo ili tawala mchezo kuanzia dakika ya 1 hadi 90.
Makosa yaliyotokea katika mchezo huo bado yameonyesha ni tatizo la taifa lote la Tanzania. Dunia ya sasa mpira ni kuweka chini na kuanza kucheza lakini haina maana kama utaishia kucheza mpira na kushindwa kufunga magoli kutokana na nafasi ulizotengeneza.
Tatizo kubwa la timu na washambuliaji wa Tanzania ni kushindwa kuzitendea haki nafasi ambazo zinapatikana. Kwa yeyote aliyetazama mchezo wa Serengeti Boys ataungana nasi Mtembezi Sports katika ili,hasa pale vijana walipotengeneza nafasi nyingi za kufunga na kuishia kukwamisha mipira mitatu tu wavuni.
Ukubwa wa tatizo ili umeonekana kipindi hiki cha karibuni hata kwa timu zetu za ligi kuu. Yanga safu yao ya ushambuliaji inaongozwa na wachezaji wa kigeni(Ngoma na Tambwe). Simba wapo na Kiiza tena bado wanaongeza na wengine. Azam kuna Kipre Tchetche. Hatuaminiki tena katika ili na hata kama mchezaji akitokea hawezi kufanya jambo hilo mfululizo. Yuko wapi Msuva yule mfungaji bora msimu wa mwaka juzi!?
Tuwasaidie Serengeti Boys kwenye tatizo ili la taifa. Kizazi chao bado wana mengi ya kujifunza kama watatiliwa mkazo katika ukuaji bora unaofuata misingi.

No comments