ELIAS MAGURI AIKACHA SIMBA NA KUSAINI MIAKA MITATU OMAN
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania na Klabu ya Stand United Elias Maguri amesaini mkataba wa miaka mitatu kukipiga katika ligi kuu nchini Oman.
Maguri ambaye alikua akiwindwa na timu yake ya zamani Simba kwaajili ya msimu ujao ameamua kuangalia kimataifa zaidi na kukubali kutimkia nchini Oman kujaribu bahati yake kusakata soka la kulipwa.
Maguri amejiunga na klabu ya Dhofar SC yenye makazi yake mjini Salalah nchini Oman kwa mkataba huo wa miaka mitatu akiwa mchezaji huru baada ya kukamilisha mkataba wake na Stand United.
Mchezaji huyo mzaliwa wa Musoma mwenye miaka 24 ni tegemeo katika safu ya ushambuliaji ya Timu ya Taifa ya Tanzania atakua na klabu yake hiyo mpya ambayo inashiriki katika michuano ya ubingwa wa Asia wakitumia uwanja wao wa nyumbani Al-Saada
Timu hiyo ilishika nafasi ya 5 katika msimamo wa ligi kuu ya Oman msimu uliopita.
No comments