TOTTENHAM YAMNG'ANG'ANIA LACAZETTE

Tottenham hotspur imeanza tena mazungumzo ya kumsajili mkali wa mabao toka Olympic Lyon ya Ufaransa Alexandre Lacazette.


Kiasi cha paundi milioni 25 kimetengwa na Spur kwaajili ya mchezaji huyo ambaye wamekua wakijaribu kumsajili mara kadhaa na kushindikana.

Baada ya kupata nafasi ya kushiriki ligi ya mabingwa Ulaya msimu ujao tayari kocha Mauricio Pochettino ameshaweka mikakati ya kufanya vizuri na Lacazette ameonekana kama mmoja kati ya nyota wanaofaa kufanya kazi hiyo upande wa ushambuliaji.

Lacazette aliyefunga mabao 23 msimu uliopita akiwa na Lyon inasemekana amefurahia kusikia habari za kuhamia White Hart Lane.


No comments

Powered by Blogger.