THE GUNNING MACHINE : ASANTE ROSICKY, ADUI YAKO AMENINYANG'ANYA MPAKA NYONGEZA.
Na Richard Leonce
Nina mahaba ya dhati kabisa na jezi namba saba ya Arsenal kuanzia wakati ikivaliwa na Robert Pires hadi iliporithiwa na Tomas Rosicky mwaka 2006. Hawa wote hawakuniangusha na walikua vipenzi vyangu. Msimu ujao ataivaa Alexis Sanchez na ninaona dalili pia kwamba hatoniangusha.
Wasomaji wangu leo nimeamua kuachana na zile stori za usajili kwanza kwa sababu hakuna jema huko. nimetoka mtandaoni kusoma habari ikisema Juventus wanajiandaa kuleta ofa ya kumsajili Alexis Sanchez, bila shaka tutawakatalia ili Sanchez avae namba 7 msimu ujao. Kwingineko, Besiktas wamekata tamaa ya kumsajili David Ospina kwa sababu ya ada yake.
Hebu tuyaweke yote pembeni tumzungumzie Tomas Rosicky leo. Jina lake huwa linaleta tabu kwenye matamshi, lakini kwa usahihi linatamkwa Rozitski. Unapata picha gani ninpomtaja?
Mimi napata picha ya dhuluma. Kuna shetani anaitwa majeraha amenidhulumu sana utamu wa Rosicky. Tangu asajiliwe kutoka Borussia Dortmund miaka 10 iliyopita amekua akiandamwa na majeraha mara kwa mara.
Japo yeye si wa kwanza kukumbana na kadhia hiyo, lakini kuna tofauti kubwa ya kimtazamo kwa mashabiki wengi wa Arsenal wanapomzungumzia Tom. Wengi tunamzungumzia kama fundi wa mpira, mtaalamu wa kupiga pasi mwenye uwezo wa kuumiliki mpira na kuutenda atakavyo.
Ni kweli Rosicky ni fundi. Ataupokea mpira, atageuka nao upande huu, ataukanyaga, atauachia, atageukia upande ule, ataukanyaga tena, atakimbia nao, atawapiga chenga mabeki wawili kwa kasi, atatoa pasi, atafunga. Ataburudisha macho yako hadi utamani kumwona tena, lakini ikifika mechi ijayo utaambiwa ameumia na atakua nje kwa miezi kadhaa.
Uncle Tom aliteka hisia za kila mpenda soka. Alipendeza na mpira kuanzia kichwani hadi miguuni. Arsene Wenger aliwahi kusema kama unapenda soka, basi unampenda Tomas Rosicky.
Ameondoka Arsenal ikiwa ni miaka 10 tangu asajiliwe. Alikuja akiwa na umri wa miaka 25, anaondoka akiwa na umri wa miaka 35. Ni nadra kwa mchezaji kudumu Arsenal mpaka umri huo. Arsenal siyo Juventus, wachezaji wa Arsenal wakifika miaka 30 tu huanza kupokea mikataba ya mwaka mmoja mmoja, jambo ambalo huwaudhi na wengi huamua kuondoka zao.
Lakini Rosicky amedumu. Ni matumaini yangu kwamba kama si majeraha angeweza kuendelea kuwepo. Siyo Arsene Wenger, wala siyo shabiki yeyote wa Arsenal na hata baadhi ya vilabu vingine ambaye alitamani Rosicky aondoke sasa hivi katika ligi kuu. Lakini haikua na jinsi mbele ya adui MAJERAHA.
Unafanya nini?
Baada ya kumsubiri kwa zaidi ya nusu ya msimu, anarejea uwanjani Januari 30 mwaka huu kwenye mchezo wa kombe la FA dhidi ya Burnley. Kila mtu anapiga makofi kwa heshima na furaha akijua utamu wa Rosicky umerudi, lakini anacheza kwa dakika 20 na kuumia tena.
Mwenyewe alitoa machozi wiki moja baadae wakati akisema, "Ni kitu ambacho bado ni kigumu kuamini kama kimenitokea mimi japo ni wiki nzima imepita sasa. Ni ngumu kwa sababu nilijiandaa vizuri kurejea, sikudharau chochote kwenye matibabu yangu.
Walimu wa viungo wamefanya kazi kubwa kunirejesha uwanjani lakini bahati mbaya nimepata tena tatizo lingine na ninapaswa kuwa nje kwa muda mwingine mrefu"
Rosicky hakuwahi kukata tamaa, pamoja na hali hiyo ngumu, aliendelea kuamini kwamba atarudi kumalizia kifurushi chake.
Nimemkumbuka ghafla Abou Diaby ambaye adui huyu huyu anaemwondoa Rosicky ndiye alimwondoa na yeye pia. Lakini tofauti kubwa na Rosicky ni kwamba Diaby yeye hakua kipenzi cha wengi.
Wakati machozi yakiwalengalenga mashabiki wakati huu wa Rosicky kuondoka, wengi walifurahishwa na kuondoka kwa Diaby wakiamini wametua mzigo.
Mimi najua sababu. Sababu ni viwango vya hawa wachezaji wawili. Diaby hakua na kiwango cha kufanya watu wamkumbuke sana alipokua na majeraha tofauti na Rosicky ambaye kila alipopata nafasi ya kucheza alikonga nyoyo haswa. Alipokua fit alithibitisha kwamba yeye ni hai pale kwenye eneo la kiungo. Huwa naukumbuka ule ubora wake akicheza na Cesc Fabregas na Samir Nasri, japo walikua hawatwai vikombe lakini walikua wakicheza mpira wa hali ya juu sana.
Rosicky ameishi Emirates akishuhudia vijana wengi wakikua kutoka academy na kua wachezaji wakubwa. Mwenyewe anasema, "Hawa akina Oxlade, Wilshere, Iwobi, Coquelin, Ramsey, Bellerin wamekua pembeni yangu. wengine walikua watoto kabisa lakini sasa wanaishi ndoto zao, nadhani kuna mchango wangu pia"
Francis Coquelin anasema mara nyingi alikua akimwona Rosicky akipiga gitaa lake huku akiwa rafiki wa kila mtu klabuni.
Naye Laurent Koscielny anasema, "Kabati lake lipo pembeni ya kabati langu, yeye ni kaka kwangu kwa hiyo kila nilipomtazama kupitia kioo wakati tunabadili mavazi nilijua sipaswi kufanya makosa ninapocheza na kaka yangu"
Huyu ndiye Tomas Rosicky, siwezi kumwacha aende hivi hivi bila kumwandika. Wakati anaagwa kwa ushindi dhidi ya Aston Villa akisema kwa heri ngumu na yenye machozi. Wachezaji wote wakivaa jezi yake kumuenzi, nilijua sitomwona tena akicheza, lakini kumbe alipanga kutupatia nyongeza kwenye Euro 2016 huko Ufaransa.
Nia yake imetimia, ametupatia nyongeza yetu kwa kiwango bora kabisa kwenye michezo miwili lakini bado la kufa ni la kufa tu, Adui majeraha alikuja tena kwenye mchezo wake dhidi ya Croatia na akamchukua tena, asante sana Rosicky, sioni ulichobakiza
twitter: @chardboy77
0766399341

No comments