USAJILI BONGO : YANGA YAMSAJILI KIPA WA PRISONS NA BEKI WA MTIBWA. SIMBA WAKO ZIMBABWE

Tetesi za usajili wa wachezaji kwaajili ya msimu ujao wa ligi kuu Tanzania bara unaendelea ambapo macho na masikio yako kwa timu kubwa za Tanzania.
Na kama ilivyo kawaida ya www.wapendasoka.com tumekuwekea hapa habari za usajili wa wachezaji hapa Tanzania.


Dante akikabana na Tambwe

YANGA

Mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara wao wameendelea kujiweka sawa kwaajili ya msimu ujao na michuano ya kimataifa.

Kupitia kwa msemaji wake Yanga imefanikiwa kuwasajili Kipa namba moja wa Prisons ya Mbeya Beno Kakolanya ambaye alikua akiwaniwa pia na Simba kwa ada ya uhamisho milioni 35 ikisemekana kuwa atakamata mshahara wa milioni moja kwa mwezi.
Kakolanya akiwa kazini
Pia Yanga imefanikiwa kuongeza beki wa kati na safari hii wakimsajili beki wa Mtibwa Vicent Andrew maarufu kama Dante ambaye anaenda Yanga kupigania namba katika kikosi ambacho tayari kina wachezaji watatu walio katika kiwango cha juu kwa nafasi ya kati.

SIMBA

wekundu wa Msimbazi Simba baada ya kupoteza makali yao na kufanya vibaya katika michuano mbalimbali wakiambulia nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi kuu ya Vodacom wao usajili wao bado umebaki ni tetesi.

Simba inamwania kocha wa timu ya taifa ya Zimbabwe Kalisto Pasuwa kuja kujaza nafasi ya kocha mkuu wa timu hiyo na tayari Mwenyekiti wa Usajili wa Simba Zacharia Hans Pope akiwa na wajumbe wa kamati ya usajili Said Tully na Colins Frisch wako Zimbabwe kwaajili ya mazungumzo na kocha huyo.

Pia Simba inamwania kocha wa Zamani wa Azam FC Patrick Omog kuja kama hawatampata kocha huyo wa Zimbabwe.

Kwa upande wa wachezaji tayari Simba inawawania wachezaji kadhaa wa ndani na nje akiwemo beki wa kati wa Malawi Harry Nyirenda anayekipiga katika klabu ya Black Leopards ya Afrika Kusini.

Kwa leo ni haya tu tukutane siku nyingine katika tetesi za Usajili wa wachezaji hapa Bongo.

No comments

Powered by Blogger.