COPA AMERICA: ARGENTINA YAWAADHIBU MABINGWA WATETEZI CHILE, PANAMA YAILIPUA BOLIVIA

Mabingwa wa michuano ya kombe la mataifa ya America maarufu kama Copa America timu ya taifa ya Chile jana ilianza vibaya harakati za kutetea ubingwa wao kwa kufungwa bao 2-1.


Chile walikubali kichapo hicho kutoka kwa Argentina moja ya nchi zinazopewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa michuano hiyo mwaka huu.

Angel di Maria na Ever Banega ndiyo waliokua mashujaa wa Argentina wakifunga mabao hayo mawili huku Chile wakipata bao la kufutia machozi kupitia kwa Jose Fuenzalida

Katika mechi nyingine ya kundi hilo C Panama waliinyuka Bolivia kwa bao 2-1 matokeo ambayo hayakutegemewa na wengi.

Magoli ya Panama yakifungwa na Blas Perez aliyefunga magoli yote mawili huku Bolivia wakipata bao pekee lililofungwa na Juan Carlos Arce.

Michuano hiyo itaendelea tena usiku wa kuamkia kesho kwa saa za hapa nyumbani ambapo Wenyeji Marekani watacheza na Costa Rica mchezo utakaoanza saa 9 alfajiri na Colombia watacheza na Paraguay mida ya saa 11 na nusu alfajiri ikiwa ni michezo ya mzunguko wa pili.

No comments

Powered by Blogger.