STAND UNITED YASAJILI WAPYA 14,WAKO WAWILI WA KIGENI.CHANONGO AONGEZA MIAKA MIWILI
Uongozi wa Klabu ya Stand United ya Mjini Shinyanga inayodhaminiwa na kampuni ya uchimbaji madini ya ACACIA Imetangaza majina ya wachezaji 14 iliyokwisha wasajili mpaka sasa kwaajili ya ligi kuu msimu ujao na michuano mbalimbali.
Wachezaji hao 14 wataungana na wachezaji wengine watakaobaki katika kikosi cha Stand United waliokua wakitumika msimu uliopita tayari kwaajili ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu Tanzania bara.
Tayari Uongozi wa Stand United umeshakamilisha taratibu za usajili wa wachezaji hao na wote wamesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Stand United wakiwemo wachezaji wawili kutoka nje ya nchi.
Lengo la usajili uliofanyika ni kuwa na kikosi imara na kuleta upinzani katika ligi kuu Tanzania bara na michuano ya kombe la shirikisho.
Uwezo wa kucheza namba zaidi ya moja pia imekua ndiyo kigezo kikubwa kwa wachezaji hao kupata nafasi ya kuitumikia Stand United msimu ujao
Orodha kamili ya wachezaji hao,namba wanazocheza na timu walizotoka ni pamoja na :-
Yusuph Sabo(Coastal union) anacheza namba 10,8,9..
Hassan Mpilipili (Toto Africans) anacheza namba 4,5,6.
Jerome Sina(Rayon Sports ya Rwanda) anacheza namba 9.
Nurdin Mganga(Mgambo Jkt) anacheza namba 5.
Benedictor Jacob(Lupopo fc-Congo) anacheza winga.
Hassan Salum(Coastal union).
Mussa Kirungi(Toto African) anacheza kama kipa.
Saleh Abdallah(Kagera Sugar) anacheza namba 2.
Jamal Mchauro(Azam fc) anacheza namba 9 au 10..
Sami Ally Nuhu(JKU-Zanzibar) anacheza namba 3.
Fehi Abdulrahman(Mafunzo-zanzibar) anacheza namba 8...
Hassan Salum(Simba SC)
Zablon Anatai(Kagera Rangers),
Najim Salum(Changanyikeni fc)
Pia Stand United imemsainisha mkataba mpya wa miaka miwili mshambuliaji wake nyota Haruna Chanongo.
Kikosi cha Stand United kitaingia katika kambi rasmi itakayoanza tarehe 1 Julai jijini Dar Es Salaam na tarehe 1 hiyo hiyo Uongozi utamtaja kocha mpya wa timu ambaye atakua na jukumu la kukinoa kikosi cha Stand.
Asanteni
Imetolewa na
ALEXANDER SANGA
MKURUGENZI WA HABARI NA MAWASILIANO
STAND UNITED COMPANY LIMITED
0715052491

No comments