ROBERTO MARTINEZ AKARIBIA KUJIUNGA NA ANDERLECHT YA UBELGIJI

Aliyekua kocha mkuu wa Everton Roberto Martinez anaendelea na mazungumzo na klabu ya Anderlecht ya Ubelgiji ili kuchukua nafasi ya kuwa kocha wa timu hiyo.



Martinez mwenye miaka 42 alitimuliwa Everton baada ya matokeo mabaya msimu uliopita katika ligi kuu ya England na alikua na mazungumzo na wawakilishi wa Anderlecht jijini Brussels katika hotel ya  Steigenberger jana Juamatano.

Anderlecht watacheza katika michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya msimu ujao wakianzia katika hatua ya mtoano baada ya kumaliza ligi ya Ubelgiji wakiwa katika nafasi ya pili.


No comments

Powered by Blogger.