RASMI : MANCHESTER CITY YAMSAJILI GUNDOGAN TOKA DORTMUND

Klabu ya Manchester City imethibitisha kumsajili kiungo wa kimataifa wa Ujerumani na klabu ya Dortmund Ilkay Gundogan.



Gundoganambaye ameachwa katika kikosi cha Ujerumani kilichotangazwa juzi kwaajili ya fainali za mataifa ya Ulaya Euro 2016 ameaaini mkataba wa miaka minne akiigharimu Man City paundi milioni 21

Mchezaji huyo anaingia katika historia ya kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na kocha mpya wa Man City Pep Guadiola ambaye ataanza rasmi kazi Julai Mosi.

Gundogan amekua akihusishwa na Manchester City kwa kipindi kirefu akitakiwa pia na klabu za Manchester United na Barcelona.

Kuwasili kwa Gundogan kunafanya idara ya kiungo ya City kuwa na viungo watano na pengine hii inaweza kupelekea kuondoka kwa nyota kadhaa kama Yaya Toure ambaye anawindwa na Leicester City.

No comments

Powered by Blogger.