EURO 2016 : WENYEJI UFARANSA WAANZA NA USHINDI

Michuano ya kombe la mataifa ya Ulaya Euro 2016 imeanza jana katika nchi ya Ufaransa kwa mechi ya Ufunguzi baina ya wenyeji Ufaransa na Romania.



Ufaransa waliweza kuibuka na ushindi wa bao 2-1 katika mchezo huo ambao Ufaransa walibanwa vilivyo na kushindwa kabisa kuonyesha makeke yao kutokana na ubora uliopo katika kikosi chao.

Dimitri Payet ndiye aliyekua shujaa wa mchezo huo baada ya kufunga goli zuri sana dakika 1 kabla ya mchezo kumalizika wakati ambao wengi walitegemea mchezo ungemalizika kwa sare ya bao 1-1 baada ya goli la kwanza la Olivier Giroud na kusawazishwa na Bogdan Stancu kwa njia ya penati.

Kama hukupata muda wa kutazama mchezo huo unaweza kuangalia highlights hapa


No comments

Powered by Blogger.