AFRICAN LYON YAKANA KUTAKA KUUTUMIA UWANJA WA MKWAKWANI

Moja kati ya timu zilizopanda daraja kutoka  ligi daraja la kwanza ambayo itacheza katika ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara klabu ya African Lyon imekanusha taarifa za kutumia uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga kwaajili ya mechi zao za ligi kuu.

 Akiongea na Wapenda Soka Mmiliki wa timu hiyo Rahim Zamunda Kangezi amesema taarifa zinaoenea katika mitandao kwamba klabu hiyo ina mpango wa kuhamishia mechi zake za nyumbani  katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga si za kweli.

Kangezi amesema hakuna sababu ya kuipeleka timu mbali ya Temeke ambako ndiko iiliposajiliwa na wananchi,wapenzi na mashabiki wa klabu hiyo wategemee kuiona timu yao ikicheza hapa hapa Dar es Salaam.

Kumekua na taarifa zinazosambaa mitandaoni zikiitaja African Lyon kutumia uwanja wa mkwakwani kufatia kushuka daraja kwa timu zote za Tanga.

No comments

Powered by Blogger.