EURO 2016 : SLOVAKIA YAIADHIBU RUSSIA (+Video Highlights)

Russia wamekumbana na kisiki baada ya kukubali kichapo cha bao 2-1 toka kwa Slovakia katika mchezo wa pili wa kundi B uliopigwa katika dimba la Pierre-Mauroy jijini Lille nchini Ufaransa.


Matokeo haya yanawafanya Russia kubaki na pointi moja tu baada ya sare yao ya bao 1-1 na England Jumamosi

Mchezaji wa zamani wa Manchester City Vladimir Weiss alitangulia kuifungia Slovakia dakika ya 32 kabla ya straika wa Napoli Marek Hamsik hajafunga bao la pili dakika ya 45 huku Russia wakipata bao la kufutia machozi dakika ya 80 likifungwa na Denis Glushakov

Tumekuandalia highlights za mchezo huo kama hukupata muda wa kuutazama 



No comments

Powered by Blogger.