EURO 2016 LEO : URENO vs POLLAND HAYA NDIYO MAMBO YA MSINGI KUYAFAHAMU KUELEKEA MCHEZO HUO

Mechi za robo fainali za michuano ya kombe la mataifa ya Ulaya Euro 2016  zitaanza kuchezwa leo kwa Ureno kuumana na Poland mchezo utakaoanza majira ya saa 4 usiku kwa saa za hapa nyumbani.


Kuelekea katika pambano hilo tumekuwekea hapa baadhi ya mambo ambayo unapaswa kuyafahamu kuhusu pambano hilo.

  • Hii ni mara ya 3 kuzikutanisha timu hizo katika mechi za kimataifa Poland wakishinda 1-0 katika mechi ya mwaka 1986 katika kombe la dunia huku Ureno ikishinda 4-0 katika mchezo wa mwaka 2002 katika kombe la dunia.
  • Hii ni mara ya kwanza Poland wanafika katika robo fainali katika michuano mikubwa tangu mwaka 1982 wakati walipofika katika hatua ya nusu fainali kombe la dunia 
  • Poland ndiyo timu pekee ambayo imetinga katika hatua ya robo fainali ikiwa na uwiano mdogo kabisa wa magoli ya kufunga ikifunga magoli matatu pekee wakifungwa goli moja.
  • Ureno na Poland ndizo timu pekee ambazo zimefikia hatua ya Robo fainali katika Michuano hiyo mfululizo tangu mwaka 1996.
  •  Ureno ndiyo nchi pekee katika michuano hiyo kucheza mechi nyingi zaidi bila kushinda kombe hilo wakicheza mechi 32.
  • Ureno ndiyo timu pekee ambayo imepata kadi chache uwanjani katika michuano ya mwaka huu kuliko timu zote zilizotinga hatua ya robo fainali.
  • Cristiano Ronaldo ndiye mchezaji pekee katika historia ya michuano hiyo aliyecheza mechi nyingi zaidi kuliko mchezaji yeyote.
  •  Ronaldo amebakiza goli moja tu kufikia rekodi ya gwiji wa zamani wa Ufaransa Michel Platini ambaye alifunga magoli 9.

www.wapendasoka.com




No comments

Powered by Blogger.