EURO 2016 : ENGLAND HALI MBAYA YATUPWA NJE NA ICELAND
England imekua timu ya mwisho kuaga katika hatua ya 16 ya mashindano yanayoendelea ya Euro 2016 nchini Ufaransa.
England imefungwa bao 2-1 na timu ya taifa dogo kabisa ya Iceland mechi ambayo imeshuhudia England wakicheza soka lisiloeleweka na lisilo na mipango
Nahodha wa England Wayne Rooney ambaye alicheza kama kiungo alitangulia kuipatia England bao la uongozi dakika ya 4 tu ya mchezo kwa njia ya penati baada ya Raheem Sterling kuangushwa katika eneo la hatari.
Ragnar Sigurdsson akaisawazishia Iceland dakika 2 baadae kabla ya Kolbeinn Sigthorsson hajaongeza la pili na kuwapa ushindi huo Iceland ambao wanashiriki michuano hiyo kwa mara yao ya kwanza katika historia.
Kwa matokeo hayo Iceland itacheza dhidi ya wenyeji Ufaransa katika mechi ya Robo fainali siku ya Jumapili.

No comments