COPA AMERICA : CHICHARITO AIPELEKA MEXICO ROBO FAINALI, URUGUAY YATOLEWA

Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Javier Hernandez Chicharito usiku wa kuamkia leo alikua mmoja wa mashujaa wa Mexico katika michuano inayoendelea ya Copa America.

Chicharito ambaye anaichezea Bayer Leverkusen ya Ujerumani alifunga bao moja katika ushindi wa bao 2-0 walioupata Mexico dhidi ya Jamaica huku goli lingine likifungwa na Oribe Peralta dakika ya 81 ya mchezo huo.

Katika mechi nyingine ya kundi hilo la C Venezuela nao walitinga hatua ya Robo fainali baada ya kuwafunga Uruguay kwa bao 1-0 goli pekee la mshambuliaji wa West Brom Jose Rondon Gimenez na kuitupa nje Uruguay ambayo ilikua ikipewa nafasi ya kuchukua ubingwa huo.

No comments

Powered by Blogger.