CARICK ASAINI MKATABA WA MWAKA MMOJA ZAIDI KUICHEZEA MANCHESTER UNITED

Kiungo wa kimataifa wa England anayeichezea klabu ya Manchester United Michael Carrick amesaini mkataba wa mwaka mmoja zaidi kuichezea Klabu hiyo inayotumia uwanja wa Old Trafford.



Carick amesaini mkataba wa mwaka mmoja jana Alhamisi mkataba ambao utamweka klabuni hapo mpaka Juni 2017.

Carick mwenye miaka 34 hivi sasa ameshaichezea Manchester United kwa miaka 10 akishinda ubingwa wa ligi kuu mara ,FA Cup mara 1,Kombe la Ligi mara 1, FIFA club World Cup mara 1na Ligi ya mabingwa ulaya mara 1.

Baada ya kusaini tu Carick alitupia picha yake katika Twitter na Instagram akiwa anabusu kombe la FA




No comments

Powered by Blogger.