AUBAMEYANG NDIYE MCHEZAJI BORA KABISA BUNDESLIGA 2015/16

Nahodha wa Gabon na mshambuliaji wa Borussia Dortmund  Pierre-Emerick Aubameyang amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa wa mwaka wa Bundesliga.


Aubameyang amemshinda mpinzani wake mkuu mshambuliaji wa Bayern Munich The Gabon Robert Lewandowski ambaye ndiye aliyeibuka kuwa mfungaji bora wa msimu uliopita.

Aubameyang ambaye ni mchezaji bora wa Africa alifunga magoli 25 na kutoa assist 6 katika michezo 31 ya ligi kuu ya Ujerumani akiisaidia Dortmund kushika nafasi ya pili .

Amefunga kwa ujumla magoli 39 katika mashindano yote msimu uliopita akiweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kushinda tuzo hiyo toka Afrika.

Ni mmoja kati ya wachezaji watatu wa Dortmund kuingia katika kikosi bora msimu katika Bundesliga akiwa pamoja na Henrikh Mkhitaryan  na Matts Hummels.

No comments

Powered by Blogger.