YAYA TOURE AKATAA OFA YA MSHAHARA KUFURU TOKA CHINA ANOGEWA NA EPL

Kiungo wa kimataifa wa Ivory Coast na Manchester City Yaya Toure amekataa ofa ya mshahara mnono toka moja ya timu tatu katika ligi kuu ya China iliyotaka kumsajili nia ni kuendelea kubaki Katika ligi kuu ya England.


Kiasi cha paundi milioni 30 kama uhamisho na paundi 577,000 kwa wiki baada ya kodi kama mshahara kilishatengwa na klabu ya ligi kuu ya China Jiangsu Suning moja kati ya klabu 3 zilizokua zikimwania nyota huyo.

Kwa mshahara huo Yaya Toure angekua mchezaji wa tatu kulipwa pesa nyingi baada ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.

Yaya Toure amebakiza msimu mmoja katika mkataba wake na Manchester City na wadadisi wa maswala ya soka wanasema Yaya hatakua na nafasi katika kikosi cha kocha Pep Guadiola kutokana na maelewano mabaya  baina yao yaliyopelekea Yaya Toure kuuzwa mwaka 2010 kwa dau la paundi milioni 24 kwenda Manchester City wakati huo Pep Guadiola akiwa kocha wa Barcelona.

Yaya Toure ameamua kuendelea kubaki na kumalizia mwaka wake mmoja ndani ya Manchester City akikataa pia ofa ya kujiunga na kocha wake wa zamani Roberto Mancin katika kikosi cha Inter Milan.


1 comment:

Powered by Blogger.