YANGA YATINGA HATUA YA MAKUNDI KOMBE LA SHIRIKISHO, DIDA SHUJAA

Mabingwa wa Ligi kuu ya Tanzania bara na wawakilishi pekee waliobaki katika michuano ya kimataifa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati Yanga ya Dar es Salaam imetinga hatua ya  makundi ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika.


Haikua kazi rahisi kwa Yanga kutinga hatua hiyo baada ya kuambulia kichapo cha bao 1-0 toka kwa Sagrada Esperanga  katika mechi ya marudiano iliyopigwa jioni ya jana huko Angola.

Licha ya kufungwa bao hilo moja bado Yanga wameweza kusonga mbele kutokana na ushindi wa bao 2-0 katika mechi ya awali jijini Dar es salaam.

Shukrani nyingi ziende kwa kipa wa Yanga na timu ya Taifa ya Tanzania Deo Munishi baada ya kupangua penati ya dakika za mwisho ambayo Sagrada waliipata katika mchezo huo ambao Nadir Haroub Cannavaro alitolewa nje kwa kadi nyekundu.

No comments

Powered by Blogger.