LIVERPOOL YACHAPWA BAO 3 NA MABINGWA SEVILLA FAINALI YA EUROPA LEAGUE

Mabingwa wa michuano ya Europa League klabu ya Sevilla ya Spain imetetea ubingwa wake baada ya kutoa kichapo cha bao 3-1 wakiifunga Liverpool ya England



Mchezo huo wa fainali ya michuano hiyo ulipigwa katika dimba La St Jacob mjini Basel Uswisi jana usiku.

Daniel Sturadge alitangulia kuifungia Liverpool bao kipindi cha kwanza bao ambalo lilidumu mpaka mapumziko

Kipindi cha pili Sevilla waliamka na kusawazisha bao hilo kupitia kwa Kevin Gameiro kisha Coke Moreno akafunga bao mbili kuipa ushindi wa bao 3-1 Sevilla na kufanikiwa kushinda ubingwa huo kwa mara ya tatu mfululizo.

Kama hukuangalia mechi hiyo unaweza kuangalia highlights hapa



No comments

Powered by Blogger.