YANGA YAKABIDHIWA KOMBE KWA SARE NA NDANDA

 Mabingwa wa ligi kuu ya Vodacoma Tanzania bara Yanga ya Dar es Salaam imekabidhiwa kombe lao la 26 walilotwaa msimu huu kwa Sare ya bao 2-2 dhidi ya wenyeji Ndanda FC


Mchezo huo wa pili kutoka mwisho kwa Yanga ulipigwa katika dimba La Taifa Jijini Dar es salaam lakini Bado Ndanda FC ya Mtwara waliendelea kuwa wenyeji katika pambano hilo

Ndanda walitangulia kupata bao la kuongoza likifungwa kwa njia ya penati na Omary Mponda kabla ya Yanga hawajaamka na kusawazisha bao hilo kupitia kwa Simon Msuva na badae Donald Ngoma akafunga bao la pili na kufanya mchezo huo kwenda mapumziko Yanga wakiwa mbele kwa bao hizo 2-1.

Kipindi cha pili Ndanda walicharuka na kucheza Kandanda safi na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha likifungwa na Salum Minelly  bao ambalo lilifanya mchezo huo kumalizika kwa Sare ya bao 2-2.

Baada ya mchezo huo ilifata shughuli maalumu ya kukabidhiwa kombe na shughuli hiyo ilifanywa na Waziri wa Kilimo Mheshimiwa Mwigulu Nchemba.

No comments

Powered by Blogger.