U-SCHOLES WA CARRICK NA UKIMYA WA MANCHESTER UNITED.
Mara nyingi thamani ya kitu huwezi kuijua hadi pale unapokuwa hauna. Ndivyo ilivyo katika dunia yetu sisi wanadamu.
Mara ya moja Xabi Alonso aliporejea Uingereza katika mechi ya kirafiki kati ya Hispania na Uingereza alisema kuna jambo linamsikitisha ni jinsi ambavyo makocha wa Uingereza walivyoshindwa kumtumia Michael Carrick katika timu hiyo ya Simba Watatu. "Ni mtu mpole ambaye kazi yake inaonekana anapokuwa uwanjani. Nikimwangalia kama najiona mimi,angekuwa Mhispania angepata nafasi sababu ni mtu ambaye anaendana nasi". Inahitaji akili ya ziada kufahamu alichokielezea Xabi Alonso juu ya Carrick,lazima uwe na ubongo mpana.
Wakati Sir Alex Ferguson anamsajili Carrick mwaka 2006 alisema hakika huyu ni kijana mwenye kipaji mwenye bahati ya kucheza Manchester United. Wakati huo huo unaambiwa Arsene Wenger alijaribu kumfatilia zaidi ya miaka miwili ili amsaini katika timu yake ya Arsenal.
Kiuhalisia Carrick ni kiungo mshikaji "Holding midfielder" ambaye anacheza kwa kuwalinda watu wanne wa nyuma yake. Holding midfielder ni tofauti na kiungo mkabaji ambaye anatumia nguvu nyingi kuzuia wapinzani. Aina ya wachezaji wa Carrick wanatumia uwezo walionao kumsoma mpinzani anavyocheza,uwezo wa kufanya tackling sahihi na uwezo wa hali ya juu wa kupiga pasi.
Carrick anafahamika na wengi kwa kupiga pasi lakini kazi zake nyingi zimekuwa zinafunikwa na uwezo wake huo wa kupiga pasi. Faida nyingine kubwa ya Carrick anakuwa anacheza kama kiungo muongo mchezeshaji "deep-lying playmaker" ambaye amekuwa anapeleka shida kwa wapinzani kwa kusukuma mipira kwa kupitia pembeni,katikati na hata kwa pasi za kupenyeza. Ambaye pia Ana uwezo wa kuzuia presha ya wapinzani "high tempo" na kuwapoozesha na kuwacommand kucheza anavyotaka yeye.
Ufanyaji kazi wa Carrick wa sasa unatia mashaka sababu ya umri wake kusonga na amekuwa muhanga wa majeruhi mara kwa mara lakini pamoja na kuwa hayupo kwenye ubora wake Man United wameendelea kumtegemea. Pamoja na uwepo wakina Schneiderlin na Schweinsteiger bado hakuna anayefanya kazi kama Carrick akiwa uwanjani. Morgan ni kiungo mkabaji ambaye hana kitu cha ziada zaidi ya kuchafua mipango ya wapinzani lakini uwezo wa kusukuma mipira hana. Bastian ni yule yule anacheza kwa kupambana na kusaidia timu kushambulia lakini hana passing rate kama aliyonayo Carrick.
Takwimu hazidanganyi,Manchester United wameshinda michezo mingi ambayo Carrick yupo ndani kwa asilimia 69. Sasa ni hadi lini United wataendelea kumtegemea Carrick ambaye sasa amekuwa anaelekea ukingoni na hata mkataba wake unaenda kuisha mwisho wa msimu huu!!. Kiufundi zaidi United wanatakiwa kumfanya Carrick kuwa Pirlo wao kwa kumtafutia watu wa kumzunguka na kumpunguzia majukumu. Maisha ya United bila Carrick yanataka kufanana na maisha yale ya bila Scholes hadi aliporudishwa tena kutoka kustaafu.
"Louis van Gaal ni muumini mkubwa wa Carrick na mapenzi yake kwake yamekuwa wazi. Anachoshindwa ni kumrudisha umri wake nyuma tu hasa ukizingatia kwa mtindo ambao ameuleta pale Old Trafford unamwitaji mtu kama Carrick kusukuma gurudumu. Wachezaji kama Carrick ni wachache sana na huwezi kuona umuhimu wao hadi pale wanapokosekana kwenye timu. Carrick ndiye anayejua United wacheze vipi ili kukabiliana na mpinzani kwa sababu ni yeye ndiye muhusika mkubwa wa kuchezesha timu kwa pasi zake.
Manchester United bila Carrick inawezekana lakini kumkosa Carrick ni pigo kwa United hasa kwa kuwa yeye na Rooney ndio wachezaji waliocheza fainali tatu za UEFA za miaka ya karibuni. Ni kiongozi kwa wenzake na anafahamu vyema utamaduni wa United. Nadhani United wakimwacha Carrick aende Mzee Wenger atakuwa tayari kumkalibisha pale Emirates bila kujali umri wake sababu ni mmoja wa wachezaji wanaomtoa udenda hadi sasa.
Nasubiri kuona United itavyojengwa bila uwepo wa Carrick. Ni kama vile ilivyojengwa kiujanjaujanja na Sir Alex bila Paul Scholes. United lazima wasake mrithi wa Carrick mapema na ikiwezekana awepo kabisa kwenye timu ili asipate shida kuzoea. Kumpata aliyefanana na Carrick inawezekana au isiwezekane ni kama United walivyohangaika kumpata Scholes mpya na wakashindwa.
Na: Ayoub Hinjo
E-mail: hinjo38@gmail.com

Umenikuna sana aisee, huwa inaniuma anaposakamwa, au kulinganishwa na Bastian/Morgan! Utulivu hasa wa Man Utd mara zote unaanzia kwake, na anatukumbusha walau sehemu ndogo tu ya kazi aliyoifanya vema Scholes kwenye wakati wake! Binafsi bado namuhitaji Carrick kwa msimu mmoja wa ziada kama tu hatatokea wa kuniaminisha kuwa anaweza kuifanya kazi ya Carrick.
ReplyDelete