SIMBA YASHUSHA KIKOSI CHA "KIZALENDO" TUPU KUIVAA MAJIMAJI JIONI YA LEO

Kwa mara ya kwanza Wekundu wa Msimbazi Simba leo itajitupa katika dimba la Majimaji mjini Songea kumenyana na wenyeji wana Lizombe klabu ya Majimaji ya huko ikiwa na wachezaji wote wa kikosi cha kwanza Raia wa Tanzania


Mchezo huo wa ligi kuu ya Tanzania bara umemgharimu kocha mkuu wa Wekundu hao Jackson Mayanja raia wa Uganda kuwatumia wachezaji pekee wa Kitanzania kutokana na kuchelewa kufika Mjini Songea wachezaji wote saba wa kigeni kwa madai ya kutolipwa mishahara yao.

Tayari Simba imepoteza nafasi ya ubingwa msimu huu na matokeo ya leo itakua ni kutaka kulinda heshima na kuleta furaha kwa Mashabiki wake ambao wamekata tamaa.

Kikosi cha Simba kitakachocheza jioni ya leo ni

1-Peter Manyika Jr
2-Mohamed Fakhi
3-Hussen Tshabalala
4-Hassan Isihaka
5-Novatus Lufunga
6-Abdi Banda
7-Said Issa
8-Said Ndemla
9-Mussa Mgossi
10-Mohamed Mussa
11-Peter Malyanzi

SUB
-Robert Kissu
-Fred Antony
-Justice Majabvi
-Hussein Magila
-Said Hamis

No comments

Powered by Blogger.