TETESI ZA USAJILI BONGO : NGOMA KUTIMKIA AFRIKA KUSINI, KIPRE TCHETCHE NJIA NYEUPE YANGA
Harakati za usajili kwaajili ya msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom umeanza kwa vilabu kadhaa kuanza usajili kwa ajili ya msimu mpya wa ligi kuu ya Soka Tanzania Bara.
Tumekuletea baadhi ya habari ambazo kwasasa bado ni tetesi na majaliwa yake tutayapata kadri ya siku zinavyoendelea.
â– Mshambuliaji Donald Ngoma wa Mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara Yanga anahusishwa kutimkia nchini Afrika Kusini katika moja ya klabu inayoshiriki katika ligi kuu ya huko maarufu kama PSL.
Awali mshambuliaji huyo raia wa Zimbabwe alishapata ofa ya kununuliwa kwa kiasi cha dola 350,000 na klabu moja nchini Yugoslavia.
Ngoma amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wa sasa katika kikosi cha Wanajangwani hao na taarifa toka ndani ya Yanga zinasema uongozi hauko tayari kumwachia.
â– Wana Lamba Lamba Azam FC pengine wanaweza kukosa huduma ya mshambuliaji wake Kipre Tchetche ambaye yasemekana amepata klabu ya kuichezea nchini Omani lakini taarifa zingine za ndani zaidi zinasema Tchetche atajiunga na Yanga.
â– Mshambuliaji Jeremiah Juma wa Prisons ya Mbeya na timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars anawania kwa karibu na wekundu wa msimbazi Simba. Simba inatafuta mbadala wa Hamis Kiiza ambaye ataachwa kutokana na utovu wa nidhamu na Jeremiah anaonekana kuwa mtu muafaka katika safu ya ushambuliaji.
â– Kocha wa Zamani wa Toto African ya Mwanza Martine Glerics ameiomba Simba kumpa kikosi hicho ili arudishe makali yake. Simba inatafuta kocha mkuu wa kusaidiana na Mayanja katika benchi la ufundi.
www.wapendasoka.com

No comments