SAFARI ISIYOTEGEMEWA YA LEICESTER CITY "UNEXPECTED JOURNEY "
Zama zimebadilika kweli kweli tena kwa kasi kubwa mno. Ni kama vile navyokumbuka mistari ya Fid Q kwenye nyimbo yake ya Usinikubali haraka,alisema "Nitafurahi kama utanimwaga nikija kwa gia za mkwanja,nitarudi kujipanga ki-underground kama fungus". Ni mistari ambayo alitumia kuelezea hisia zake kwa msichana mrembo.
Fid Q ametuletea hiki kisa kupitia Leicester City ambao walibeba Mwali bila kutumia fedha kubwa kwenye uwekezaji wa wachezaji. Zama zimebadilika tena kwa Manchester United ambao wamekuwa wa kuombea fulani afungwe ili apate kushiriki michuano ya Ulaya,ni ajabu kweli. Achana na habari ya United,nadhani kila mmoja amewaona mabingwa wa ligi kuu ya Uingereza Leicester City walivyowaacha midomo wazi wapenzi na mashabiki wa mpira duniani. Kwa kifupi ilikuwa ni safari isiyotarajiwa kwao wenyewe na hata kwa Muitaliano Ranieri.
Safari hii ambayo haikutegemewa na wengi imeleta safari nyingine ambayo haitegemewi pia ya Leicester kucheza michuano ya Ulaya maarufu kama "UEFA Champions League". Hapo ndipo mengi yanazaliwa kutoka kwa wadau wa soka duniani. Kitendo cha Leicester kufuzu michuano hiyo kama bingwa wa Uingereza kinawaongezea presha ya kuwa na mashindano mengi kwa msimu mmoja tofauti na msimu ambao walitumia nguvu nyingi kupambana kwenye ligi kuu kuliko kwenye makombe mengine ya ndani "Domestic cups".
Safari hii ijayo ya Leicester ni ngumu kweli hasa kwenye kujikinga na majeruhi kutokana na ushiriki wa mashindano mengi. Kumbuka Leicester ni moja ya timu ambazo zilikuwa na majeruhi wachache pia ni timu ambayo haikuwa na mzunguko mkubwa wa wachezaji kama timu zingine "players' rotation". Nadhani ni jambo la kuanza kuangaliwa kwa jicho lingine sasa.
Safari isiyotegemewa ni hii ya kukaa na wachezaji wao mahiri kwa msimu mwingine tena. Dalili za kina Kante,Mahrez,Vardy na wengine kubaki ni ndogo hasa ukizingatia wamekuwa wakihusishwa na timu za ndoto kwao. Hakuna mchezaji wa zama hizi asiyependa kuwa katika historia ya timu kama Barcelona,Real Madrid,Bayern Munich,Arsenal,Man United na nyingine. Kama Leicester watauza wachezaji ni dhahiri waanze tena kutengeneza timu na hata kama wachezaji watabaki sidhani kama watatoa walichonacho kwa asilimia zote kama awali walivyoingia kwenye timu sababu ya uchovu.
Safari hii ni ngumu kwa Leicester hasa pale wanapokaa meza moja na timu kubwa zaidi duniani kuliko wao kuanzia historia na hata mafanikio kwa ujumla sioni kama watamudu kucheza mechi zile zenye wimbo mzuri ambao Luis Suarez ulimfanya aondoke Liverpool kwa kukosa usingizi sababu ya mawazo.
Pamoja na safari hii kuwa isiyotegemewa jaribu kumwangalia dereva aliyeifikisha Leicester hapa ilipo ndani ya muda mfupi. Anaitwa Claudio Ranieri kocha ambaye amekuwa akifundisha mpira kwa miaka 30 nini cha zaidi unataka kutoka kwake ikiwa amefundisha timu kubwa nyingi duniani!? Timu kama Chelsea,Juventus,Monaco,Inter Milan na nyingine nyingi lakini huko kote hakubahatika kushinda kombe zaidi ya kuishia nafasi ya pili,hayo ndiyo yalikuwa mafanikio yake makubwa ukiacha haya ya sasa aliyopata Leicester City. Kwa takwimu hizo ni dereva mzuri anayejua na kujali kazi yake.
Uzoefu wa Ranieri kwenye safari hii ni msaada mkubwa kwa Leicester sababu ni mtu ambaye anajua kucheza na akili ya wachezaji wake wamfanyie anachotaka kama alivyokuwa anafanya kwa kuwanunulia Pizza wanaposhinda.
Kama nilivyosema hapo awali safari hii ni kubwa na ngumu mno kwao tena inawezekana kuwa ngumu mno kuliko hata United kufuzu michuano ya Ulaya.
Na: Ayoub Hinjo
E-mail: hinjo38@gmail.com

No comments