REAL MADRID KUMKOSA VERANE FAINALI LIGI YA MABINGWA ULAYA

Taarifa za kitabibu kutoka katika kikosi cha Real Madrid zinasema kwamba mlinzi wa kati Raia wa Ufaransa Raphael Verane ataikosa mechi ya fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya siku ya jumamosi dhidi ya Atletico Madrid.


Verane anasumbuliwa na maumivu ya misuli na pengine anaweza kukosekana kwa takribani wiki 3 japokua madaktari bado wanaendelea kuangalia kwa ukaribu maendeleo ya afya yake.

Kocha Wa Real Madrid Zenedine Zidane amekua akiwatumia zaidi Sergio Ramos na Pepe katika nafasi ya kiungo huku Verane akianzia benchi.

Real Madrid watacheza na Atletico Madrid katika mechi hiyo ya fainali itakayochezwa katika dimba la San Ciro jijini Milan huku Real Madrid wakitaka kuchukua ubingwa wao wa 11 katika historia ya klabu hiyo.




No comments

Powered by Blogger.