MWADUI YAICHAPA SIMBA NA KUIPA YANGA UBINGWA LIGI KUU TANZANIA BARA
Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara Yanga ya Dar es Salaam imetawazwa rasmi kuwa mabingwa kwa mara nyingine baada ya Mwadui FC kuibuka na ushindi dhidi ya Wekundu wa Msimbazi Simba .
Simba Ikicheza katika dimba la Taifa wakiwa ni wenyeji wa Mwadui FC ya Shinyanga walijikuta wakifungwa bao 1-0 katika pambano ambalo kama Simba ingeshinda basi ingeizuia Yanga kutangaza ubingwa
Shujaa wa mchezo huo alikua ni mshambuliaji wa Mwadui FC Jamal Mnyate ambaye aliipangua vilivyo Ngome ya Simba na kufunga bao hilo pekee dakika ya 73 ya mchezo
Simba licha ya kufungwa ilimpoteza pia mshambuliaji wake tegemezi Ibrahim Ajibu aliyelambwa kadi nyekundu
Kwa matokeo hayo sasa Yanga wanatawazwa kuwa mabingwa kwani kwa michezo iliyobaki hakuna timu itakayoweza kuwafikia wakiwa kileleni na pointi zao 68.
HONGERENI SANA YANGA

No comments