AZAM FC YAICHAPA KAGERA SUGAR NA KURUDI "NAFASI YAKE"

Mabingwa wa soka Afrika Mashariki na Kati Azam FC imeigaragaza Kagera Sugar kwa bao 2-1 katika mechi za lala salama ligi kuu Tanzania bara.


Pambano hilo lilipigwa katika dimba la Kambarage mjini Shinyanga lilikua la kukamilisha ratiba tu kwa Azam FC lakini lilikua la muhimu zaidi kwa Kagera Sugar ambao sasa balaa la kushuka Daraja linanukia.

Azam FC ambayo sasa imerejea katika nafasi yake ya pili baada ya Simba kukubali kichapo dhidi ya Mwadui ilipata mabao yake kupitia kwa Himid Mao na Kipre Tchetche na kuwafanya sasa kufikisha pointi 50 pointi 8 nyuma ya Yanga na 2 mbele ya Simba.

No comments

Powered by Blogger.