MANCHESTER CITY NA NDOTO YA KUCHEZA FAINALI LIGI YA MABINGWA ULAYA, INAPAMBANA NA REAL MADRID LEO
Ndoto ya Manchester City kucheza katika Katika fainali yao ya kwanza ya ligi ya Mabingwa barani Ulaya yaweza kutimia leo watakapokabiliana na Real Madrid ya Spain katika dimba la Santiago Bernabeu jijini Madrid.
Manchester City itaingia katika pambano la leo wakihitaji Sare ya magoli au ushindi kuweza kutinga katika fainali ya tarehe 20 Mwezi huu dhidi ya Atletico Madrid baada ya mechi ya awali kumalizika kwa Sare ya bila kufungana.
Kwa upande wa Real Madrid wao watakua na faida ya kucheza katika dimba lao la nyumbani Santiago Bernabeu huku changamoto pekee ikiwa ni kufunga na kuwazuia Man City kufunga na ushindi pekee ndiyo utaivusha Real Madrid.
Cristiano Ronaldo ambaye ni mfungaji bora kabisa wa michuano hiyo atarejea dimbani leo baada ya kukosekana katika mechi ya awali.
Kama Real Madrid watavuka hatua hii basi watakutana na Atletico Madrid katika mechi ya fainali na kukumbushia fainali ya miaka miwili iliyopita ambapo Real walitwaa ubingwa.
Mechi hii itaanza majira ya saa nne kasorobo za usiku kwa saa za hapa nyumbani.

No comments