LICHA YA KICHAPO ATLETICO MADRID YATINGA FAINALI LIGI YA MABINGWA ULAYA

Atletico Madrid kutoka Spain imekua timu ya kwanza kutinga katika fainali ya ligi ya Mabingwa barani Ulaya jana licha ya kufungwa bao 2-1  na Wenyeji Bayern Munich ya Ujerumani.


Pambano hilo la nusu fainali ya pili La Ligi ya Mabingwa barani Ulaya lilipigwa katika dimba La Allianz Arena jijini Munich Ujerumani ambapo Atletico Madrid imetinga fainali kwa faida ya bao la ugenini baada ya kushinda bao 1-0 katika mechi ya awali.

Bayern Munich ilitatangulia kufunga kwa goli la kiungo Xabi Alonso lakini Antony Griezmann akaisawazishia Atletico Madrid kipindi cha pili kabla ya Lewandowski hajaongeza bao la pili ambalo halikuisaidia Bayern kuepuka kutupwa nje.

Katika pambano hilo timu zote zilipata penati na zote zikakosa Thomas Muller kwa upande wa Bayern Munich na Fernando Torres kwa upande wa Atletico Madrid


Sasa Atletico Madrid wataisubiri timu itakayovuka leo katika mechi ya nusu fainali ya pili baina ya wenyeji Real Madrid na Manchester City ilitinga kucheza katika fainali tarehe 20 Mwezi huu kule Milan Italia.


No comments

Powered by Blogger.