MAMBO UNAYOPASWA KUYAJUA BAADA YA MECHI ZA JUZI JUMAPILI EPL

Baada ya mechi tatu za juzi Jumapili nchini England hizi ni baadhi ya rekodi ambazo zimewekwa na yapo mengi ambayo unaweza ukawa huyafahamu.



SOUTHAMPTON 4-2 MAN CITY

  • Southampton wamefunga goli 4 au zaidi katika mechi mfululizo za Ligi kuu nchini England kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo.
  • Manchester City wao wamefungwa goli 4 au zaidi katika mechi 3 za ligi kuu msimu huu ikiwa ni mara ya kwanza tangu msimu wa mwaka 2000/2001 walipofungwa zaidi ya goli 4 ka katika  mechi 6.
  • Sadio Mane amefunga goli 7 katika mechi 6 zilizopita katika ligi kuu ya England baada ya ukame wa mechi 19 bila goli lolote.
  • Sadio Mane juzi alipiga mashuti matano golini manne kati ya hayo yakiwa on target na matatu yalizaa magoli.
  • Mane Aligusa mpira mara 72 na kufanya 8 tackles katika mchezo huo ikiwa ni mara nyingi kuliko mchezaji yeyote wa Southampton.

SWANSEA CITY 3-1 LIVERPOOL

  • Swansea juzi  walipata ushindi wao wa nne mfululizo  katika uwanja wao wa nyumbani ikiwa ni mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo na Ligi kuu nchini England.
  • Christian Benteke alifunga bao lake la 50 katika ligi kuu ya England huku Andrew Ayew akifunga mabao mawili katika mechi moja ikiwa ni mara ya kwanza tangu ajiunge na Swansea.
  • Magoli matatu waliyofunga Swansea jana ikiwa ni mara ya kwanza kwao kufunga magoli matatu katika ligi kuu ya England tangu walipofanya hivyo tarehe 25 Aprili 2015 ikiwa ni mara ya mwisho pia mchezaji Jack Cork kufunga bao na hapo juzi alifunga bao moja.

MANCHESTER UNITED 1-1 LEICESTER CITY

  • Leicester wamepoteza mchezo mmoja tu dhidi ya Liverpool katika michezo 10 iliyopita katika ligi kuu nchini England ambayo walitangulia kufungwa wakishinda mara 3 na kutoka sare 6.
  • Anthony Martial ameshafunga magoli 15 tangu ajiunge na Man United katika mashindano yote akiwa ni mchezaji pekee kufanya hivyo katika kikosi cha United msimu huu.
  • Goli alilofunga Martial jana lilikua goli la kwanza Leicester City kufungwa katika dakika 10 za mwanzo katika msimu huu.
  • Pasi ya goli aliyoitoa Danny Drinkwater jana ni pasi yake ya 7 katika msimu huu akizidiwa na James Milner mwenye assists 11, Delle Alli pasi 9 na Rose Barkley passi 8 kati ya wachezaji wa England katika ligi.
  • Kushindwa kufunga goli lolote jana dhidi ya Leicester City kunamfanya Wayne Rooney kufikisha timu tatu ambazo hajawahi kuzifunga katika mechi za Ligi kuu nchini England tangu ajiunge na Man United zingine ni Derby County na Blackpool.
  •  Claudio Ranieri ameshinda mechi 2 tu katika mechi 10 katika ligi kuu dhidi ya Man United akitoka Sare 6 na kupoteza mara 2.

No comments

Powered by Blogger.