MABINGWA WATETEZI SEVILLA WATINGA FAINALI KUCHEZA NA LIVERPOOL

Mabingwa watetezi wa michuano ya Europa League klabu ya Sevilla ya Spain imetinga fainali ya michuano hiyo kwa mara nyingine baada ya kuitoa Shaktar Donetsk kwa ushindi wa Jumla wa bao 5-3.


Sevilla ilipata mabao yake kupitia kwa Kevin Gameiro aliyefunga mabao mawili peke yake na bao moja la Mariano huku Aduardo akifunga bao pekee La Shakhtar Donetsk.

Hii ni mara ya tatu mfululizo Sevilla wanatinga fainali ya michuano hiyo na mara zote mbili zilizopita wamefanikiwa kutwaa kombe hilo na sasa wanatafuta nafasi ya kuweka rekodi mpya kwa kulitwaa kombe hilo mara tatu mfululizo.

Fainali sasa itakua kati ya Sevilla ya Spain na Liverpool ya England ambayo itapigwa katika dimba la Basle Uswis Mei 18.

No comments

Powered by Blogger.