KLOPP AENDELEA KUIWEKA LIVERPOOL SAWA, AIPELEKA FAINALI EUROPA LEAGUE

Kocha mkuu wa Liverpool Jurgen Klopp ameendelea kuionyesha dunia kwamba anataka kuirejesha Liverpool katika makali yake ya zamani kwa kuipeleka katika fainali ya michuano ya Europa League 
Katika miezi michache ndani ya Liverpool tayari tumeona mabadiliko makubwa kwa kikosi cha Liverpool huku ikionyesha soka safi na kupata ushindi muhimu tena bila hata ya kufanya usajili mpya.

Jana usiku katika nusu fainali ya michuano ya Europa League Liverpool ilihitaji ushindi wa bao  zaidi ya moja kuweza kutinga hatua ya fainali wakicheza dhidi ya Villareal ya Spain.

Liverpool iliibuka na ushindi mnono wa bao 3-0 katika mchezo huo uliopigwa katika dimba la Anfield. 

Bruno Soriano wa Villarreal alitangulia kuwapa goli Liverpool akijifunga na kufanya mchezo huo kwenda mapumziko Liverpool wakiwa mbele kwa bao hilo moja.

Kisha kipindi cha pili Daniel Sturadge na Adam Lallana wakaongeza bao moja moja na kufanya Liverpool kuzoa pointi zote tatu muhimu na kufuzu fainali kwa Jumla ya bao 3-1.

Hii ni nafasi nyingine sasa kwa Live kushiriki michuano ya ligi ya Mabingwa barani Ulaya mwaka I kama watafanikiwa kutwaa kombe hilo.

Unapaswa kujua kwamba katika fainali 11 ambazo Liverpool wamecheza katika michuano ya Ulaya, wameshinda 8 na 5 katika hizo ni katika ligi ya mabingwa Ulaya huku 3 zikiwa ni za UEFA Cup.

No comments

Powered by Blogger.