LIVERPOOL KUPINDUA MATOKEO LEO? INACHEZA NA VILLARREAL EUROPA LEAGUE

Mechi za marudiano hatua ya nusu fainali ya michuano ya Europa League zitachezwa leo usiku katika viwanja viwili barani Ulaya.


Jijini Liverpool wenyeji jogoo  wa jiji klabu ya Liverpool itakua na shughuli pevu kutaka kupindua matokeo ya awali ya bao 1-0 kule Spain watakapokabiliana na Villareal katika dimba la Anfield.

Ushindi pekee na kuzuia wasifungwe  bao ndiyo silaha ya Liverpool kutinga katika fainali ya michuano hiyo ambayo bingwa wake atapata pia nafasi ya kushiriki katika michuano ya ligi ya Mabingwa barani Ulaya

Mechi nyingine leo ni ile itakayozikutanisha mabingwa watetezi Sevilla watakaokua nyumbani kuwaalika Shakhtar Donetsk ya Ukraine.

Pambano la awali kule Ukraine lilimalizika kwa Sare ya bao 2-2 matokeo yanayoipa faida Sevilla kwani Shakhtar wanatakiwa kushinda au kupata Sare ya zaidi ya bao 3 ili wapite.

Mechi zote hizo zitaanza saa nne na dakika 5 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

No comments

Powered by Blogger.