LIGI KUU TANZANIA BARA LEO : SIMBA IKO MOROGORO, AZAM TANGA

Baada ya jana kushuhudia mabingwa Yanga walikabidhiwa kombe lao leo ligi hiyo ya Vodacom Tanzania bara itaendelea kwa mechi kadhaa kupigwa wengine wakikamilisha ratiba na kulinda heshima lakini wengine wakiwa katika vita ya kutoshuka daraja.



Mjini Morogoro wenyeji Mtibwa sugar watakua wakiwakaribisha Wekundu wa Msimbazi Simba katika mechi itakayopigwa katika dimba la Jamhuri.


Mechi ya awali baina ya timu hizo Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0 goli pekee La Hamis Kiiza mchezo uliopigwa katika dimba la Taifa jijini Dar es salaam

Jijini Tanga leo Wenyeji African Sports watakua na shughuli pevu ya kutaka kubaki katika ligi kuu watakapowaalika Wana lamba lamba Azam FC toka jijini Dar es salaam na ushindi pekee katika mchezo huo ndiyo silaha ya kusabakisha katika ligi

Huko Shinyanga leo kutakua na mechi mbili Mwadui FC watacheza na Mbeya City huku Stand United wakicheza na Kagera Sugar wakati kule Mbeya Prisons wataialika Toto Africans ya Mwanza.



No comments

Powered by Blogger.