LEO KATIKA HISTORIA : BARCELONA YAFUTA NDOTO ZA MAN UNITED KUTETEA UBINGWA WA UCL MWAKA 2009

Leo katika historia tunakumbuka fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya kati ya Barcelona na Manchester United tarehe 27 Mei 2009 katika dimba la Olimpico jijini Roma Italia.



Kocha wa Manchester United Sir Alex Ferguson baada ya kuiongoza klabu hiyo kushinda ubingwa wa ligi ya mabingwa barani Ulaya mwaka 2008  alifanikiwa tena kuiongoza Man United kutinga fainali kwa mara ya pili mfululizo na ikitaka kuwa klabu ya kwanza kutetea ubingwa wa Ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Ndoto hizo zilizimwa na kikosi cha kocha Pep Guadiola ambacho kilifanikiwa kuifunga Manchester United kwa bao 2-0 vikosi vyote viwili vikisheheni nyota kadhaa kwa Upande wa Man United walikua na mchezaji bora wa dunia wakati huo Cristiano Ronaldo na upande wa Barcelona wakiwa na Lionel Messi.

Samuel Eto'o alitangulia kufunga bao la kwanza kisha Lionel Messi akaongeza la pili kwa kichwa na kumwacha kipa wa United Van De Sir asiwe na la kufanya na kufuta kabisa ndoto za United kutetea taji hilo.

Kiukweli kikosi cha Barcelona kilikua bora sana usiku huo kwa muda wote wa mchezo japokua United walijitahidi kuliandama lango la Barcelona kipindi cha kwanza

VIKOSI VILIKUA HIVI.

BARCELONA

Valdes, Puyol, Toure Yaya, Pique, Sylvinho, Xavi, Busquets, Iniesta (Pedrito 90), Messi, Eto'o, Henry

Wachezaji wa akiba ambao hawakutumika:
Pinto, Caceres, Muniesa, Gudjohnsen, Bojan.

Man Utd: 

Van der Sar, O'Shea, Ferdinand, Vidic, Evra, Anderson (Tevez 46), Carrick, Giggs (Scholes 75), Park (Berbatov 66), Ronaldo, Rooney.

Wachezaji wa akiba ambao hawakutumika:
 Kuszczak, Rafael Da Silva, Evans, Nani.

Watazamaji: 72,700
Refa: Massimo Busacca (Switzerland)



No comments

Powered by Blogger.