BAADA YA KUBEBA MAKOMBE YOTE, WACHEZAJI YANGA WAPEWA LIKIZO YA WIKI MOJA
Uongozi wa mabingwa wa soka wa Tanzania bara na wawakilishi pekee wa kimataifa Yanga imewapa mapumziko ya wiki moja wachezaji wake wote.
Akizungumza na www.wapendasoka.com Afisa habari wa klabu hiyo ambayo pia ni mabingwa wa kombe la Shirikisho Jerry Muro amesema wachezaji wamepewa wiki moja kwenda kusalimia familia zao baadae watarejea kambini tayari kwaajili ya kujiandaa na michezo ya makundi hatua ya robo fainali katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika.
Jerry alisema "Lengo kuu lao kwa sasa ni kuona wanatinga hatua ya nusu fainali na hatimae fainali na hata usajili wao unalenga zaidi kuimarisha kikosi hicho kwaajili ya michuano hiyo"
Yanga wamekua na msimu mzuri kabisa kuwahi kutokea kwa klabu hiyo baada ya kushinda ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara na ule wa shirikisho na kutinga hatua ya robo fainali kombe la shirikisho barani Afrika.

No comments