KADI ZATAWALA BARCELONA IKIBEBA KOMBE LA COPA DEL REY

Mabingwa wa Spain Barcelona jana walishinda ushindi wao wa pili msimu huu kwa  kutwaa kombe la mfalme nchini Spain maarufu kama Copa del Rey wakiwafunga Sevilla kwa bao 2-0.


Mchezo huo wa fainali ulipigwa katika dimba la  Vicente Calderón jijini Madrid ambapo zilishuhudiwa kadi nyingi zikitolewa kufuatia timu hizo kufanyiana madhambi muda wote.

Jumla ya kadi 13 za njano na kadi 3 nyekundu zilitolewa katika mchezo huo ambao ilibidi uchezwe mpaka dakika za nyongeza kufuatia kwenda sare ya bila kufungana mpaka dakika 90 zinamalizika.

Neymar na beki wa Pembeni Jordi Alba walifunga mabao

No comments

Powered by Blogger.