FAINALI YA LIGI YA MABINGWA ULAYA LEO : MAMBO MUHIMU UNAYOPASWA KUYAJUA
Fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya inachezwa leo katika jiji la Milan katika uwanja wa San Ciro baina ya timu za mji mmoja wa Madrid yani Atletico Madrid watakaocheza dhidi ya Real Madrid.
Fainali hii ni marudio ya Fainali ya mwaka 2014 baina ya timu hizo na Real Madrid kuchukua ubingwa wao wa 10 katika historia ya michuano hiyo ikiifunga Atletico kwa bao 3-0.
Mambo mengi yameandikwa kuhusu mchezo huu wa leo lakini www.wapendasoka.com imeamua kujikita kukupa mambo adimu ambayo unapaswa kuyajua kuhusu pambano hilo.
Fainali hii ni marudio ya Fainali ya mwaka 2014 baina ya timu hizo na Real Madrid kuchukua ubingwa wao wa 10 katika historia ya michuano hiyo ikiifunga Atletico kwa bao 3-0.
Mambo mengi yameandikwa kuhusu mchezo huu wa leo lakini www.wapendasoka.com imeamua kujikita kukupa mambo adimu ambayo unapaswa kuyajua kuhusu pambano hilo.
- Real Madrid wamefunga magoli 110 na kufungwa magoli 34 katika ligi ya Spain msimu huu wakati Atletico Madrid wao wamefunga magoli 63 tu lakini wamefungwa magoli 18 pekee hii ina maana Real Madrid wana safu nzuri ya ushambuliaji wakati Atletico Madrid wao wameonekana wana safu bora ya Ulinzi.
- Cristiano Ronaldo ndiye kinara wa Real Madrid akiwa amefunga au kutoa assist sawa na 74% ya magoli yote ya Real Madrid katika ligi ya mabingwa msimu huu amefunga mara 16 na kusaidia mara 4 katika magoli 27 ya Real Madrid.
- Antoine Griezmann ndiye kinara kwa upande wa Atletico Madrid akiwa ameshiriki kwa 55% ya magoli ya Timu hiyo katika ligi ya mabingwa barani Ulaya akifunga magoli 7 na kusaidia goli 1 katika magoli 16 waliyofunga Atletico katika michuano hiyo msimu huu.
- Cristiano Ronaldo amekuwa na msimu wa sita mfululizo wa mafanikio katika klabu yake akiwa amefunga tayari magoli 51 katika mashindano yote msimu huu na kumfanya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga magoli zaidi ya 50 katika misimu 6 mfululizo katika La liga akiwa ameshafunga magoli 16 katika mechi 11 za michuano hii ya ligi ya mabingwa Ulaya.
- Licha ya kuzifumania nyavu kwa kiwango hicho lakini bado Ronaldo ameshindwa kuwafunga Atletico Madrid katika michezo mitano iliyopita.
![]() |
Real Madrid wakishangilia ubingwa wao wa 10 mwaka 2014 |
- Wakati Real Madrid wanaingia katika mchezo wa leo wakitaka kuchukua ubingwa wao wa 11 wa ligi ya mabingwa Ulaya Atletico Madrid wao wanapigania kupata ubingwa wao wa kwanza katika historia ya michuano hiyo baada ya kushindwa kufanya hivyo mara 2 walizofika fainali.
- Real Madrid watacheza fainali ya leo ikiwa ni fainali yao ya 14 ikiwa ni klabu ya kwanza kufanya hivyo na katika hizo 13 zilizopita wameshinda mara 10 wakishinda fainali zao 4 zilizopita
- Hii ni mara ya tatu katika misimu minne ya fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya inashindanisha timu kutoka katika nchi moja (Germany 2013, Spain 2014, Spain 2016)
- Jiji la Madrid ndilo linaloongoza kwa kutoa timu nyingi zilizofika fainali ya michuano hiyo likifanya hivyo mara 17 ikiwa 14 za Real Madrid na 3 za Atletico Madrid na Jiji la Milani Linafatia kwa kutoa timu shiriki katika fainali 16.
- Atletico Madrid wameshinda mechi 7 kati ya 16 zilizopita dhidi ya Real Madrid katika mashindano yote wakitoka sare mara 5 na kufungwa mara nne.
- Hii ni mara ya 3 mfululizo katika fainali za ligi ya mabingwa barani Ulaya mmoja wa makocha wanaofika fainali ndiyo mara yake ya kwanza katika timu husika (Diego Simeone 2014, Luis Enrique 2015, Zinedine Zidane 2016).
No comments