DIMITRI PAYET AIOKOA UFARANSA NA GOLI LA DAKIKA YA MWISHO.

Kiungo wa Kimataifa wa Ufaransa na klabu ya West Ham ya England Dimitri Payet jana alikua shujaa katika ushindi wa bao 3-2 dhidi ya Cameroon.


Ufaransa ambao ni  waandaaji wa michuano ya Euro 2016 inayotarajiwa kuanza Juni 10 Mwaka huu waliikaribisha Cameroon katika mchezo wa maandalizi wa michuano hiyo katika juji la Nantes.

Dimitri Payet alifunga goli la ushindi kwa mpira wa adhabu ndogo dakika ya 90 ya mchezo baada ya timu hizo kuwa sare ya bao 2-2 mpaka muda huo kufuatia goli la dakika ya 87 walilopata Cameroon kupitia Kwa Eric Choupo Moting.

Blaise Matuidi na Olivier Giroud walitangulia kuipatia Ufaransa mabao mawili ya awali huku Cameroon wakipata bao la kwanza kupitia kwa Vicente Aboubakar.

No comments

Powered by Blogger.