MATAMSHI YA FERGUSON YAMPA VAN GAAL MKATABA MPYA KUIFUNDISHA UNITED MPAKA 2020
Baada ya kunukuliwa na vyombo vya Habari kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson akiwaomba mashabiki wa klabu hiyo kumpa muda kocha Louis van Gaal hatimaye uongozi wa klabu hiyo umeamua kumpa mkataba mpya kocha wake huyo.
Van Gaal anatazamiwa kusaini mkataba mpya leo Ijumaa wakati wa mazoezi ya timu hiyo katika viwanja vya mazoezi vya AON na baadae ataongea na waandishi wa Habari kuhusu kwa nini ameongeza mkataba huo lakini pia atazungumzia mchezo wa wikiend hii dhidi ya Everton.
Mkataba wa kocha huyo Mdachi ndani ya United unatazamiwa kuisha msimu ujao na kwa kuongeza mkataba huo mpya wa miaka mitatu basi Atadumu mpaka mwaka 2020.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo Ed Woodward amesema "Tumeamua kumpa LVG mkataba mpya baada ya kuona maendeleo katika kikosi hasa kwa kuwapa nafasi vijana ambao wanazalishwa na klabu yetu"
Hii si Habari njema kwa mashabiki wa United kwani tayari wengi walishamchoka kocha huyo huku kukitawala tetesi nyingi zinazomuhusisha Jose Mourinho kujiunga na klabu hiyo mwishoni mwa msimu.
No comments