YANGA YARUDI KILELENI KWA JEURI YAIPIGA AFRICAN SPORTS "MKONO"

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya soka Tanzania bara Yanga imerudi tena kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo inayodhaminiwa na  Vodacom Tanzania Kwa kuitandika bila huruma African Sports ya Tanga bao 5-0.





Mchezo huo ulipigwa katika dimba la Taifa jijini huku Yanga wakionekana kuwaelemea vilivyo African Sports ambao wamepanda kucheza ligi kuu msimu huu na mpaka mapumziko tayari Yanga ilishaweka kambani bao 2-0.

Mlinzi wa Yanga  Kelvin Yondani alitangulia kuifungia bao la kwanza klabu yake kabla ya Donald Ngoma hajaongeza la pili.

Kipindi cha pili African Sports walifunguka na kutaka kurudisha mabao hayo mawili na ndipo dhahama ilipowakuta Kwa kufungwa bao 3 zaidi Amiss Tambwe akifunga mara mbili na Mzanzibari Mateo Antony akifunga bao moja kukamilisha ushindi  huo

Kwa matokeo hayo Yanga sasa wanarejea kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo wakifikisha pointi 50 na kuwaacha Simba wakiwa na pointi 48 katika nafasi ya pili huku Azam FC wakishika nafasi ya tatu na pointi zao 47.

No comments

Powered by Blogger.