GARETH BALE AREJEA DIMBANI KUMSAIDIA RONALDO KUIVUSHA REAL MADRID LEO USIKU
Baada ya kuwa majeruhi Kwa muda mrefu winga na mshambuliaji wa Real Madrid Gareth Bale Leo anatarajia kuanza katika mchezo wa pili wa ligi ya mabingwa barani Ulaya hatua ya 16 bora dhidi ya AS Roma katika dimba la Santiago Bernabeu.
Real Madrid itaingia katika mchezo wa Leo ikiwa na mtaji wa bao 2-0 walizopata katika mchezo wa awali kule Roma hivyo kuhitaji sare to katika mchezo wa leo kuweza kutinga hatua ya robo fainali. Cristiano Ronaldo akifunga bao moja na moja lingine likifungwa na Jese Rodriguez katika mchezo wa awali.
Gareth Bale aliingia akitokea benchi katika mchezo wa ligi kuu nchini Spain Jumamosi na kufunga bao 1 katika mabao 7-1 Real Madrid waliyoshinda dhidi ya Celta Vigo na kutoa matumaini Kwa kocha Zinedine Zidane
Katika mechi nyingine leo usiku Wolfsburg ya Ujerumani itakua nyumbani kucheza na mabingwa wa Ubelgiji Gent. Katika mchezo wa awali kule Ubelgiji Wolfsburg walishinda 3-2

No comments