YANGA NA AZAM KATIKA MTIHANI WA KOMBE LA SHIRIKISHO LEO
Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) linatarajiwa kuendelea leo kwa michezo miwili kuchezwa katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo
Azam
FC watakua kwenye uwanja wa Azam Complex kuwakaribisha maafande wa
Tanzania Prisons siku ya Alhamis saa 10 jioni kwa saa za Afrika
Mashariki.
Young
Africans watakua wenyeji wa Ndanda FC katika uwanja wa Taifa jijini Dar
es salaam, huku kila timu ikihitaji ushindi katika michezo hiyo ili
kuweza kufuzu kwa hatua ya nusu fainali.
Aprili
11, Simba SC watakamilisha hatua ya robo kwa fainali kwa kucheza na
wagosi wa kaya Coastal Union katika uwanja wa Taifa jijini Dar es
salaam.
Mwadui FC ndio timu pekee mpaka sasa ambayo imeshafuzu kwa hatua ya nusu fainali, baada ya kuwachapa Geita Gold kwa mabao 3 -0.
Bingwa
wa michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup)
atawakilisha Tanzania mwakani kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho
barani Afrika (CAF CC) mwaka 2017.
No comments