TRA YAING'NG'ANIA TFF, YAKAMATA MAGARI YAKE YOTE KUYAPIGA MNADA WASIPOLIPA KODI
Deni la Shilingi za Kitanzania 1.1Bilion limesababisha mamlaka ya Mapato nchini TRA kukamata magari matano ya shirikisho la Soka nchini Tanzania (TFF) jana deni linaloelezwa kuwa ni la mwaka 2010 mpaka mwaka 2015.
Richard Kayombo ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Elimu na Huduma kwa Walipa Kodi wa TRA, amethibitisha kukamatwa magari hayo na hivi sasa yamehifadhiwa katika Yard ya magari ya Yono Action Mart ya jijini Dar es Saalm.
Ikumbukwe kwamba tayari TRA walishawahi kuzifungia akaunti za TFF kutokana na kushindwa kulipa kodi kwa makocha wa kigeni na wafanyakazi wa shirikisho hilo.
Kayombo amesema zoezi hilo ni endelevu na tayari walishatoa taarifa TFF kwa maandishi juu ya kufuatwa masharti ya kukomboa magari yao, endapo watashindwa kulipa basi yatauzwa, yote hayo yamebainika baada ya kufanya ukaguzi.

No comments