VPL LEO ~ SIMBA IKO MKWAKWANI KUWAVAA COASTAL UNION

Vinara wa ligi kuu nchini Tanzania Wekundu wa Msimbazi SIMBA leo Jumamosi watakua jijini Tanga kucheza na wenyeji Coastal Union ya huko katika mfululizo wa mechi za ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.



Simba itaingia katika mchezo wa leo ikiwa katika hali nzuri baada ya kuendeleza ushindi katika mechi zake na kuiweka kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa na pointi 54 pointi 4 zaidi ya Yanga na Azam wanaoshika nafasi za pili na tatu wakifunga na kwa pointi kila timu ikiwa na pointi 50.

Mchezo uliopita Simba ilishinda bao 1-0 ikiifunga Tanzania Prisons wakati Coastal Union wao walifungwa bao 4-0 na Kagera Sugar.

Mechi zingine za leo Majimaji watawakaribisha Mbeya City katika dimba la Majimaji pale Songea wakati Stand United watakua nyumbani Kambarage kuwaalika Ndanda FC ya Mtwara.

No comments

Powered by Blogger.