SHOMARI KAPOMBE APIGA BAO 2 AZAM FC IKITINGA NUSU FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO

Kasi ya kufunga ya beki wa kimataifa wa Tanzania na Azam FC Shomari Kapombe imeendelea leo baada ya kufunga magoli mawili katika ushindi wa
magoli 3-1 waliopata Azam FC dhidi ya Tanzania Prisons.




Shomari Kapombe aliipa uongozi timu yake baada ya kufunga bao la kuongoza kabla ya Jeremiah Juma hajaisawazishia Prisons na kufanya mchezo huo kwenda mapumziko timu zikiwa sare ya bao 1-1.

Kipindi cha pili kilikua kichungu kwa Wajelajela hao kutoka Mbeya kwani Shomari Kapombe alifunga bao lake la pili huku Hamis Mcha akifunga naye bao moja na kuifanya Azam FC kuwa timu ya tatu kutinga NUSU fainali baada ya Mwadui na Yanga kutangulia tayari katika hatua hiyo.

No comments

Powered by Blogger.