PENATI YA YONDANI YAIPELEKA YANGA NUSU FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO

Beki wa kati wa kimataifa wa Tanzania anayeichezea Yanga ambao ni mabingwa wa Tanzania bara Kelvin Yondani leo aliibuka shujaa baada ya kuifungia timu yake bao muhimu katika mechi ya kombe la Shirikisho nchini Tanzania.




Yanga iliibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Ndanda FC ya Mtwara katika pombano la robo fainali lililopigwa katika dimba la Taifa jijini Dar es Salam.

Paul Nonga alitangulia kuifunga Yanga bao la kwanza akiunganisha kwa kichwa mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na Mlinzi Juma Abdul lakini Ndanda waliweza kusawazisha kupitia kwa mchezaji wa zamani wa Yanga na Simba Kiggy Makassy akiipangua beki ya Yanga na kuachia mkwaju mkali uliomshinda kipa wa Yanga Deo Munishi.

Kwa matokeo hayo Yanga inaungana na Mwadui FC na Azam FC kutinga NUSU fainali ya michuano hiyo ambayo Bingwa wake ataiwakilisha nchini katika kombe la Shirikisho Africa.

No comments

Powered by Blogger.